RC Simiyu ahubiri upendo, ushirikiano kwa vyama vya siasa

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi, ameongoza vyama vya siasa vya upinzani 19 mkoani Simiyu kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo, pamoja na kupata nao chakula cha pamoja.

Katika ziara hiyo RC Kihongosi amewasisitiza viongozi wa vyama vya siasa Simiyu kudumisha umoja, upendo na mshiakamno katika mkoa huo kwa kuzingatia kuziishi 4R za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

RC Kihongosi ametumia fursa hiyo kuwaeleza viongozi wa vyama vya siasa mkoani Simiyu kuwa yeye na viongozi wenzake wameteuliwa na Rais Dkt. Samia kuwatumikia wananchi na miradi yote wanayotekeleza ni yakwao na kwa kuwa ni yakwao ni lazima waijue.

“Lazima viongozi wa siasa mjue miradi imegharimu shilingi ngapi, lakini pia mjue kuwa miradi hii inakwenda kutatua shida za wananchi wenu mnaowaongoza katika jamii, kwahiyo nyinyi mtusaidie kwenda kuwatuliza wananchi mkahubiri amani,” amesema Kihongosi



Chapisha Maoni

0 Maoni