Rais Samia kuondoka nchini eo kuelekea Marekani

 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini leo Oktoba 29 kuelekea Des Moines, lowa, nchini Marekani kuhudhuria Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug ulioandaliwa na Taasisi ya World Food Prize Foundation ya nchi hiyo.

Mjadala huo hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na viongozi, wataalamu, watu mashuhuri, watunga sera, hususan za kilimo, lishe na usimamizi wa rasilimali.

Lengo la majadiliano hayo ni kutafuta suluhu ya changamoto ya upatikanaji wa chakula duniani, ambayo inachochewa na mabadiliko ya tabianchi.

Chapisha Maoni

0 Maoni