Rais Samia apongezwe kwa kukamilisha mradi wa SGR- Kikwete

 

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete amesema Rais Samia Suluhu Hassa anapaswa kupongezwa kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, huku vipande vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Akijibu swali la Idriss Sultan katika Podcast maalumu iliyofanyika nyumbani kwake, Rais huyo wa awamu ya nne wa Tanzania, amesema kuwa wazo la SGR lilianza baada ya Mkapa kufanya mazungumzo na Rais Kagame wa Rwanda juu ya kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Kigali.

Hata hivyo Kikwete amesema tumpongeze Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi huo utakaogharimu takriban Dola bilioni 7 za kimarekani.

Chapisha Maoni

0 Maoni