Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Taasisi ya JKCI kwa
kuanzisha kitengo cha kuhudumia magonjwa ya moyo Zanzibar katika Hospitali ya
Mkoa Lumumba.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo wakati akifunga kongamano hilo
la Wataalamu wa Kimataifa wa magonjwa ya moyo liloandaliwa Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete JKCI na Wizara ya Afya Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya
Golden Tulip Airport lililowashirikisha Wataalamu wa Afya ndani na nje ya
nchini.
Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali kuwekeza katika vifaa vyote
vya matibabu ya Moyo Zanzibar.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameagiza Wizara ya Afya Zanzibar
kuanza haraka majadiliano na Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI ili
huduma za upasuaji wa moyo zianze kutolewa Zanzibar kipindi kifupi
kijacho.
Rais Dk. Mwinyi pia amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itatenga rasilimali zilizopo ili kuendeleza juhudi za utafiti, kinga
na matibabu ya magonjwa ya moyo.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi amesema dhamira ya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha huduma za Afya kwa kutoa
matibabu ya magonjwa ya moyo na kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika.
Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amewahimiza wananchi kutumia vyakula vinavyoshauriwa na wataalamu pamoja na kufanya mazoezi.
0 Maoni