Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),
Jecha Salim Jecha amefariki dunia katika Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam leo
Julai 18, 2023.
Jecha atakumbukwa kwa kufuta uchaguzi mkuu Zanzibar wa mwaka
2015, jambo lililoibua mtafaruku na kumpatia umaarufu mkubwa nchini.
Taarifa zilizotofikia hii leo zinasema taratibu za mazishi
zinaendelea kufanywa mabapo imeelezwa kuwa mwili wake utapelekwa Zanzibar kwa
maziko.
Mwaka 2020, Jecha alichukua fomu ya kugombea urais wa
Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini hakufanikiwa kupewa ridhaa.
0 Maoni